Fainali ya FA kupigwa Uwanja wa Mkwakwani.
Meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya fainali ya mchezo wa kombe Shirikisho la Azam utakaochezwa katika dimba hilo.
Na Denis Chambi, Tanga.
Mkoa
wa Tanga umepokea kwa furaha kubwa taarifa za kutangazwa kuwa mchezo
wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam utachezwa katika dimba la
CCM Mkwakwani kwa msimu huu wa 2022/2023.
Meneja
wa uwanja CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' alisema wamepokea kwa
bashasha taarifa hizo kuona kwamba uwanja wao unakidhi vigezo vya
kuchezwa fainali hizo huku akiahidi kwenda kuyafanyia marekebisho baadhi
ya maeneo ambayo bado hayajakaa sawa kulingana na hadhi ya mashindano
hayo.
"Hii
ni fursa kubwa sana ambapo tunategemea kupata mashabiki wengi kutoka
wilaya za mkoa wetu na kutoka mikoa mingine tofauti tofauti kuja
kuangalia fainali hii katika mkoa wetu wa Tanga kwetu ni fursa kubwa ,
kuna viwanja vingi sana lakini huu ndio umechaguliwa hatuwezi kukubali
fursa hii itupite"
"
Toka kuanza kutangazwa kwa uwaja wa Mkwakwani kwetu huu ni mkakati
namba moja kwa maana ya kwamba zile sehemu zote ambazo ni korofi kwa
upande wetu sisi tunapaswa kuzishughulikia ipasavyo katika eneo la
Pitch tutaendelea kuliboresha na mengine kwa sababu fainali hii ni
kubwa tutakaa kama kamati kuona baadhi ya maeneo gani ambayo tuweza
kuanza nayo lakini pia kuyashughulikia ndani ya wakati" alisema Nassa.
Alisema
kuwa licha ya wapezi mashabiki na wadau wa soka kupokea taarifa hizo
kwa furaha itakuwa pia ni fursa ya kipekee siku hiyo itakayofungu
mlango kwa watu mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kutokana na uwepo
wa watu tofauti wa kutoka nje na ndani ya mkoa huo.
"Licha
ya Mashabiki wengi kuja Mkwakwani kushuhudia fainali hizi lakini pia ni
fursa kwa watu wengine wakiwemo wafanyabiashara, watu wa usafiri,
wauzaji wa vyakula pamoja na wengineo wengi kila mwana Tanga kwa namna
yake ni fursa kwake. Alisema Nassa.
Hatua
ya robo fainali ambayo itaanza kuchezwa March 31 hadi april 2,2023 kwa
timu ta Simba SC kukutana na Ihefu , Azam FC wao watachuana na Mtibwa
Sugar Singida wakiminyana Mbeya City na mchezo wa mwisho utawakutanisha
Yanga SC dhidi ya Geita Gold kutafuta tiketi ya kutinga nusu
fainali..

Comments
Post a Comment