MELI KUBWA ZA MIZIGO ZAENDELEA KUTIA NANGA BANDARI YA TANGA
Meli ya mizigo yenye urefu wa mita 179 ambayo imekuja na magari kutoka china China ikiwa ni mara ya kwanza kushushwa magari bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 450. Meneja wa bandari ya Tanga Masoud Mrisha akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Wazitri Kindamba mara baada ya kufanya ziara yake ya siku moja kutembelea bandarini hapo march 15,2023. Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya kutembelea bandari ya Tanga kushoto kwake ni meneja wa bandari hiyo Masoud Mrisha. Na Denis Chambi, Tanga. Matokeo chanya ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika bandari ya Tanga yanaendelea kuonekana kufwatia meli kubwa za mizigo kutoka nje ya nchi zikiendelea kutia nanga wafanyabiashara wakizidi kuitumia hatua ambayo inakwenda kuongeza biashara shindani katika ukanda wa Afrika mashariki. Ukiachana na meli kubwa iliyopokelewa hivi karibuni...