BUHURI TANGA YAWAPA ELIMU WAFUGAJI WA NG'OMBE MUHEZA JUU YA BORA YA UZALISHAJI WA MAZIWA .
Na Denis Chambi,Tanga. WIZARA ya mifugo na Uvuvi iko mbioni kuja na mradi wa kuwakopesha wafugaji Ng'ombe wa maziwa hapa nchini hii ikiwa na dhamira Serikali ya kuwasaidia kuondokana na ufugaji wa mazoea ili waweze kupata faida zaidi. Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua semina ya kuwapa elimu wafugaji wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga iliyoandaliwa na Wakala wa mafunzo ya Mifugo LITA kampasi 'BUHURI' kwa lengo la kuwapatia njia bora ya kutumia katika kujihusisha na ufugaji wa kisasa ambapo amesisitiza ushirikiano baina ya wadau , wafugaji na serikali ili kuwezeaha kuinua zaidi sekta hiyo. Alisema wizara mifugo na uvuvi inakuja na mradi mahususi wa kuwakopesha wafugaji Ng'ombe wa kisasa wa maziwa ambao watatakiwa kulipa kupitia maziwa watakayozalisha ambapo mchakato huo utakamilika hivi karibuni Mkoa wa Tanga ukiwa ni miongoni mwa wanufaika. "Tuna mradi mwingine ambao unakuja Muheza wa 'C