Posts

BUHURI TANGA YAWAPA ELIMU WAFUGAJI WA NG'OMBE MUHEZA JUU YA BORA YA UZALISHAJI WA MAZIWA .

Image
Na Denis Chambi,Tanga. WIZARA ya mifugo na Uvuvi  iko mbioni kuja na mradi wa kuwakopesha wafugaji Ng'ombe wa maziwa hapa nchini hii ikiwa na dhamira  Serikali ya kuwasaidia kuondokana na ufugaji wa mazoea ili waweze kupata faida zaidi. Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua semina ya kuwapa elimu wafugaji wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga  iliyoandaliwa na  Wakala wa mafunzo ya Mifugo LITA kampasi 'BUHURI'  kwa lengo la kuwapatia njia bora ya kutumia katika kujihusisha na ufugaji wa kisasa ambapo amesisitiza ushirikiano baina ya wadau ,  wafugaji na serikali ili kuwezeaha kuinua zaidi sekta hiyo.  Alisema wizara mifugo  na uvuvi inakuja na mradi mahususi wa kuwakopesha wafugaji  Ng'ombe  wa kisasa  wa maziwa ambao watatakiwa kulipa kupitia maziwa watakayozalisha  ambapo mchakato huo utakamilika hivi karibuni Mkoa wa Tanga ukiwa ni miongoni mwa wanufaika. "Tuna mradi mwingine ambao unakuja  Muheza wa  'C

Jiji la Tanga lapongezwa kupata hati safi miaka mitano mfululizo.

Image
Na Denis Chambi,  Tanga. HALMASHAURI ya jiji la Tanga imepongezwa na tume ya maadili ya viongozi wa Umma  kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiyi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' ikitakiwa kuongeza usimamizi wa matumizi ya fedha pamoja na koboresha utendaji ili kuendelea kufanya vizuri. Pongezi hizo zimetolewa leo November 2, 2023 na afisa maadili kutoka tume ya maadili nchini  Zanabu Kissoky akimwakilisha mkurugenzi wa tume ya maadili ya viongozi wa Umma  wakati akiwa kwenye kikao cha  robo ya kwanza  cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Tanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kusema licha ya pongezi hizo ni lazima halmashauri iangalie na kujitathmini kupitia hoja zilizotolewa mwaka uliopita na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG'. "Nilikuwa najaribu kuangalia ripoti za ukaguzi kwa miaka mitano jiji la Tanga mnapata hati safi na  inayoridhisha niwapongeze kwa hilo lakini tunafahamu h

MELI KUBWA ZA MIZIGO ZAENDELEA KUTIA NANGA BANDARI YA TANGA

Image
Meli ya mizigo yenye  urefu wa mita 179 ambayo imekuja na magari kutoka china China  ikiwa ni mara ya kwanza kushushwa magari bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 450. Meneja wa bandari ya Tanga Masoud Mrisha akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Wazitri Kindamba mara baada ya kufanya ziara yake ya siku moja kutembelea bandarini hapo march 15,2023. Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya kutembelea bandari ya Tanga kushoto kwake ni meneja wa bandari hiyo Masoud Mrisha. Na Denis Chambi,  Tanga. Matokeo chanya ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika bandari ya Tanga yanaendelea kuonekana kufwatia meli kubwa za mizigo kutoka nje ya nchi  zikiendelea kutia nanga wafanyabiashara wakizidi kuitumia hatua ambayo inakwenda kuongeza biashara shindani katika ukanda wa Afrika mashariki. Ukiachana na meli kubwa iliyopokelewa hivi karibuni imeendelea kuwa mwendelezo

Fainali ya FA kupigwa Uwanja wa Mkwakwani.

Image
          Meneja wa uwanja wa CCM  Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya fainali ya mchezo wa kombe Shirikisho la Azam utakaochezwa katika dimba hilo.   Na Denis Chambi,  Tanga. Mkoa wa Tanga umepokea kwa furaha kubwa taarifa za  kutangazwa kuwa mchezo wa fainali  ya kombe la Shirikisho la Azam   utachezwa katika dimba la CCM Mkwakwani kwa  msimu huu wa 2022/2023. Meneja wa uwanja CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' alisema wamepokea kwa bashasha taarifa hizo kuona kwamba uwanja wao unakidhi vigezo vya  kuchezwa fainali hizo huku akiahidi kwenda kuyafanyia marekebisho baadhi ya maeneo ambayo bado hayajakaa sawa kulingana na hadhi ya mashindano hayo. "Hii ni fursa kubwa sana ambapo tunategemea kupata mashabiki wengi kutoka wilaya za mkoa wetu na kutoka  mikoa mingine  tofauti tofauti kuja kuangalia fainali hii katika mkoa wetu wa Tanga kwetu ni fursa kubwa , kuna viwanja vingi sana lakini huu ndio