Jiji la Tanga lapongezwa kupata hati safi miaka mitano mfululizo.
Na Denis Chambi, Tanga. HALMASHAURI ya jiji la Tanga imepongezwa na tume ya maadili ya viongozi wa Umma kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiyi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' ikitakiwa kuongeza usimamizi wa matumizi ya fedha pamoja na koboresha utendaji ili kuendelea kufanya vizuri. Pongezi hizo zimetolewa leo November 2, 2023 na afisa maadili kutoka tume ya maadili nchini Zanabu Kissoky akimwakilisha mkurugenzi wa tume ya maadili ya viongozi wa Umma wakati akiwa kwenye kikao cha robo ya kwanza cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Tanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kusema licha ya pongezi hizo ni lazima halmashauri iangalie na kujitathmini kupitia hoja zilizotolewa mwaka uliopita na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG'. "Nilikuwa najaribu kuangalia ripoti za ukaguzi kwa miaka mitano jiji la Tanga mnapata hati safi na inayoridhisha niwapongeze kwa hilo lakini...